Back to top

TANZANIA CHINI YA RAIS MAGUFULI IMEPANDA NAFASI MBILI JUU

05 April 2018
Share

Na OMARI KIBANGA

Juzi nilisoma kitu mahali, mTanzania mmoja aliandika Tanzania imeshuka nafasi kadhaa kwenye orodha ya nchi zinazovutia wawekezaji Africa.   Habari ile ni ya kupuuzwa na ukweli wa mambo uko hivi.

Tanzania tumepanda nafasi mbili katika ripoti ya benki ya RMB ya mwaka 2018, na kuweza kuwa nchi ya 7 Africa nzima na ya pili Africa Mashariki, kwa nchi zenye mazingira yanayovutia uwekezaji, wazungu wanaita investiment attractiveness. Hii ni habari kubwa sana kwetu kama Taifa, wawekezaji wanakuja na faida nyingi, ndugu zetu wa Makonde wanaelewa vizuri sana hili, kuweza kuwa taifa la 7 kati ya mataifa 54 ni jambo jema na lenye kutupa heshima waTanzania wote.

Habari hii unaweza kuisoma kwa kina katika link yeyote kati ya hizi mbili ninazo kuwekea hapa chini, ila nashauri msome link ya kwanza ambayo kiingereza chake kidogo wabongo mnaweza mkakielewa 

1. https://www.tanzaniainvest.com/economy/country-to-invest-in-africa-2018

2. http://www.rmb.co.za/globalmarkets/where-to-invest-in-africa-2018-edition/

Kuwa nafasi ya saba kati ya nchi 54 sio jambo jepesi, na huwezi kuwa katika nafasi hiyo kwa zali, ranking ya mambo ya muhimu kama haya, yanahusisha tafiti za maana, report kama hii sio sawa na ile inayosema watanzania hawana furaha, furaha ni kitu cha kufikirika, kinapimwaje? Lazima tujiulize, wamepima wakina nani na kutoka wapi hadi kujua hatuna furaha, isije kuwa wameenda kuhoji watu kule ndugusi kijiji cha kabanga kwa yule dogo mwenye akili nyingi aliyempeleka mzee wake polisi ili asiuze kiwanja/nyumba, halafu wanakuja wanachapisha habari eti waTanzania wote hatuna furaha. Kwa mujibu wa ile taarifa, walisema furaha tuliyonayo sisi, tumemezizidi nchi tatu tu duniani, hivi hii inawezekanaje? Huku si kucheza na akili zetu na kutuzalilisha kabisa? Kuna nchi ngapi zina vita duniani, yaani sisi wenye amani tumeshindwa hadi na nchi zenye vita?? Mambo ya ajabu kabisa haya, kupitia ripoti ile nilijifunza jambo moja, sio kila ripoti ni ripoti, ripoti nyingine hazina hata hadhi ya kuitwa magazeti ya udaku, tuzipuuze.

Turudi kwenye ripoti yetu hii inayohusu maswala yenye tija kwenye maisha ya kila mtanzania. Ripoti ambayo haitokani na waraka wowote ule, ripoti hii iliyotuweka katika nafasi ya 7 imeangalia vigezo kama Ushindani wa kimataifa, Hali ya ufisadi na rushwa ndani ya Taifa, uhuru wa kiuchumi katika taifa, nk. Wamezingatia mambo ya msingi sana.

Wawekezaji huzingatia kwa umakini wa hali ya juu ripoti kama hizi wanapofikia hatua ya kujiuliza wakawekeze wapi, hawaamui tu, wanasearch vitu kama "Where to invest in Africa". Sasa leo wakisearch wanakuta tuko nafasi ya 7 Africa na ya 2 Africa Mashariki, na ripoti hii imeeleza sababu za sisi kuweza kupanda hizo nfasi mbili vema kabisa, Usione mtu kama Bilgate anakuja Tanzania, wala usishangae kuona Tajiri yeyote Duniani akifika Tanzania, iko siku Jeff Bezos atakuja (huyu ndio Tajiri namba moja duniani kwa sasa), lakini  hawezi kuja tu, lazima aangalie mazingira ya uwekezaji yakoje kwanza, atakapofahamu tupo kwenye nafasi nzuri, kwanini asije? Kwa hili, tujipongeze kama Taifa na tuipongeze serikali iliyo madarakani. Wawekezaji wanapokuja hawaji kuinufaisha serikali peke yake, wanakuja na faida nyingi kama ajira pamoja na uboreshaji wa miundombinu mbalimbali kupitia kitu kina CSR au corporate social responsibility..

Sambamba na hilo, kwenye maelezo ya mwishomwisho kwenye ripoti hii, jina la Daktari Magufuli limetokea, mheshimiwa Rais wetu ametajwa kama kiongozi aliyeanzisha mageuzi ya kuondokana na tatizo la rushwa lakini pia kama kiongozi anayetengeneza mazingira mazuri ya usajili wa kampuni na upatikanaji wa leseni za biashara kutokuwa na longolongo.

Ripoti ikaendelea kusema, serikali imedhamiria kuongeza uzalishaji wa ndani ili kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje na kwa kufanya hivyo Tanzania itaweza kufika hali ya kipato cha kati.

Report inamaliza kwa kusema, Tanzania ni moja ya nchi chache za Africa ambazo mataifa mengi makubwa      yanatamani kufanya uwekezaji wa kimkakati, likiwemo taifa la China.

Kwa maelezo zaidi na picha unaweza kuingia kwenye link nilizokupa hapo juu.

Comments