Back to top

RC MAKONDA AWATAKA WANANCHI KUCHUKUWA TAHADHARI NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.

17 April 2018
Share

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amefanya ziara ya kuwatembelea na kuwapa pole wahanga wa mafuriko na kuwataka wananchi waishio maeneo ya mabondeni kuhama ili kuokoa maisha yao. 

RC Makonda amesema kuwa hadi sasa zaidi ya watu 7 wamepoteza maisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo ambapo amesema njia pekee iliyobaki ni wananchi kuchukuwa tahadhari. 

Kufuatia mwendelezo wa mvua hizo RC Makonda ameziomba mamlaka husika kusimamisha masomo kwa muda wa siku mbili ili kuwaepusha wanafunzi kukumbwa na Maafa. 

Aidha RC Makonda amesema serikali inaendelea na ukarabati wa miundombinu iliyoharibiwa vibaya na mvua ikiwemo madaraja, Barabara,shule pamoja na kuzibua mitaro. 

Akiwa Mtaa wa Mfaume Kata ya upanga RC Makonda ameshuhudia jengo la gorofa kumi likiwa limepata hitilafu ya kutitia ambapo ameagiza  mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina na kuwasihi wakazi wa jengo hilo pamoja na majirani kutafuta sehemu ya kujisitiri kwa wakati huu kwa mustakabali wa usalama wao. 

Pamoja na hayo RC Makonda amewahimiza wananchi kufuatilia tahadhari zinazotolewa na mamlaka ya Hali ya hewa nchini pamoja na vyombo vya habari.

Comments