Back to top

IJUE MIRADI 6 YA SEKTA YA AFYA KATIKA JIJI LA ARUSHA INAYOJENGWA KWA MPIGO

11 April 2018
Share

Zahanati mpya ya Olimoti

Zahanati mpya ya Kimandolu

Kituo cha afya cha Murieti kata ya Murieti kipo hatua ya umaliziaji

Wodi  ya akinamama ya Moivaro kata ya Moivaro ikituo cha afya Moivaro ipo hatua ya umaliziaji

Jengo la (OPD) la Hospitali ya wilaya iliyopo kata ya Engototo eneo la Njiro  lipo katika hatua ya umaliziaji

Jiji la Arusha  linajenga miradi  ya Afya kimkakati ikiwa imetawanyika pande zote ili kuwapunguzia wananchi kujazana eneo la katikati ya jiji kwenye vituo vya Kaloleni ,Ngarenaro na Levolosi na hata hospitali ya rufaa ya mount Meru,

kaskazini kuna zahanati mpya ya Kimandolu na wodi ya wazazi katika kituo cha afya cha Moivaro iliyo katika hatua ya mwisho kabisa ya kukamilika magharibi ipo zahanati ya olimoti iliyopo hatua ya mwisho kabisa ya kukamilika,

kusini kipo kituo cha afya Murieti kilichopo hatua ya mwisho kabisaya kukamilika mashariki kipo kituo cha afya Moshono kilichopo hatua ya finishing,

katikati kuna jengola wagonjwa wa nje la hospitali ya wilaya eneo la Njiro. '

Vituo vya zamani ni pamoja na  Themi, mkonoo, Levolosi,Ngarenaro,Kaloleni na daraja mbili ambavyo vikiungana na hivi vipya 7 vinavyoendelea kwa mpigo msongamano katika Vituo vyetu vya Afya katika Jiji la Arusha itakuwa sasa ni historia' alisema afisa mmoja wa ngazi ya juu wa jiji hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe.

 

 

Comments