Back to top

ZENDA: ASIFU UTENDAJI KAZI WA KATA YA CHAMAZI, AZUNGUMZIA KITABU CHA HATUBEBI MABEGI.

06 April 2018
Share

Na: Mwandishi wetu.

Upanga,  Dar es Salaam.

Alhamisi 5 April 2018.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi Ndg. Nasri Mkalipa amekutana na kuzungumza na Kaimu Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Taifa Ndg. Daniel Zenda.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Alhamisi 5 April katika ofisi ya Kaimu Katibu huyo yalipo makao makuu ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Upanga jijini Dar es Salaam. 

Mazungumzo hayo ya viongozi hao yalikuwa na lengo la kuzungumzia na kutazama masuala mbalimbali ya siasa ikiwemo Ndg. Mkalipa kupewa ushauri juu ya kuifanya jumuiya ya vijana katika Kata ya Chamazi kuendelea kuwa hai muda wote.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Ndg. Zenda aliusifu uongozi mzima wa UVCCM Kata ya Chamazi kwa kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka.

"Nimefurahi sana ujio wako katika ofisi yangu Ndg. Mkalipa niseme tu wewe ni kioo cha viongozi wengi waliopo ngazi ya Kata" alisema Zenda 

"Mambo mnayoyafanya Kata ya Chamazi kwa hakika sikuwahi kuyaona wala kuyasikia katika Kata zingine katika nchi hii, pongezi sana kwenu" alisema Zenda.

"Haipiti muda mrefu nawaona mitandaoni mara mnafanya hiki mara kile kwa hakika nyinyi ni Kata ya mfano" alisema Zenda.

Sambamba na hilo Ndg. Zenda alimpongeza Ndg.  Mkalipa kwa ubunifu na uthubutu aliouonyesha wa kuandika kitabu cha HATUBEBI MABEGI,  TUKUTANE KAZINI. 

"Siku zote nilikuwa natamani nikipate na kukisoma kitabu chako cha Hatubebi Mabegi, leo nimekipata na kukisoma kwa hakika umeandika vizuri na maneno yaliyomo humu kama vijana watakisoma na kuyazingatia watakuwa viongozi wazuri" alisema Zenda.

"Hongera sana Mkalipa na nawaomba vijana wengine nchi nzima wasikalie majungu na unafiki na badala yake wawe wabunifu kama wewe" alisema Zenda.

mabe

Comments