Back to top

WAJUMBE WA MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM WILAYA ILEMELA WAPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI

11 April 2018
Share

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula ametumia fursa hiyo pia kumshukuru aliyekuwa katibu wake Comrade Kheri James ambae sasa ni Mwenyekiti wa UVCCM (T) kwa ushirkikiano mkubwa aliyompa katika utekelezaji wa Ilani Jimboni, Aidha aliwashukuru waratibu wa ofisi ya mbunge ngazi ya kanda kwa maana ya kanda ya Bugogwa, Kirumba, Nyakato na Ofisi kuu kwa ushirikiano wao mkubwa uliowezesha mambo yote kwenda sawia.

Taarifa ya utekelezaji wa Ilani  inawasilishwa kwa kuzingatia katiba ya CCM Ibara ya 73 (3) na Ilani ya uchaguzi Ibara 180 taarifa hiyo yenye kurasa 88 imeainisha mambo mbalimbali kulingana na Sekta

Ambapo Mhe Dkt Mabula aliainisha utekelezaji huo kwa namna ambavyo Serikali kuu, Halmashauri, Mfuko wa Jimbo na Taasisi ya The Angeline Foundation kwa kushirikiana na Wadau walivyowezesha utekelezaji huo kuanza na Mfuko wa Jimbo Shilingi 106,685,600 zimetumika kutengeneza madawati 530, Shilingi 53,156,600 kuchonga barabara mpya yenye Km 27.6, Shilingi 44,500,000 kujenga Kivuko kata ya Mecco, Shilingi 4,000,000 na Ujenzi wa Kivuli cha kituo cha afya Kirumba Shilingi 5,029,000.

Huku Jumla ya shilingi 12,300,000 zikitumika katika kutoa elimu ya Ujasiriamali kwa mabalozi 1403 walipatiwa elimu hiyo na wanachama wapatao 3756 wamefundishwa ambapo Mhe Dkt Angeline Mabula alizishukuru taasisi za Intergrity Foundation na Sudama Investment kwa kuwezesha mafunzo ya wajasiriamali wakishirikiana na taasisi ya The Angeline Foundation

Upande wa sekta ya Ardhi jumla ya viwanja 15564 vimepimwa kupitia upimaji shirikishi kufikia Desemba 2017 na hati 5502 zilikuwa zimetolewa, Aidha kati ya migogoro ya ardhi yote iliyomfikia mbunge huyo, amesema asilimia 90 ya migogoro hiyo imetatuliwa na kuahidi changamoto iliyopo katika mgogoro wa airport na wananchi wa Shibula utapatiwa ufumbuzi muda si mrefu alisema Dkt Mabula

Sekta ya Miundombinu , Fedha toka Serikali kuu shilingi 500,000,000 zimetumika katika kituo cha fya Karume kujenga miundombinu yote muhimu, Huku shilingi 1,200,000,000 zikitumika kukarabati miundombinu ya barabara na madaraja fedha toka mfuko wa barabara, na kwa sasa kuna miradi 14 ya ujenzi wa barabara ambapo wakandarasi wako site na katika hatua nyengine  Dtk Mabula alifanya uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kitangiri mzunguko-Kabuhoro Ziwani yenye Km 3 ambapo Km 1.5 ya  barabara hiyo inajengwa na GeminiContractors Ltd ambapo Dkt Mabula alitoa shukrani kwa Mhe Dkt John Magufuli kwa hatua nzuri ya upanuzi wa Uwanja wa ndege, Ujenzi wa daraja la Furahisha na kutengewa fedha Bilioni 2.3 kwaajili ya ujenzi wa Kivuko cha Kisiwa cha Bezi na Kayenze.

Ili kuendana na teknolojia ya kisasa, Jumla ya kompyuta 11 zilipokelewa na kupelekwa katika vituo 3 vya afya na zahanati 7 na Kompyuta nyengine 60 zilipelekwa shule ya sekondari  za Buswelu kompyuta 20, Bwiru kompyuta  20 na Bugogwa kompyuta 20, Aidha madawati 28 yamejengwa 22 tayari na kukamilika na madarasa 6 yakiendelea kujengwa

Pamoja na hayo Mfuko wa Angeline Foundation umetumia shilingi 265,418,800 katika shughuli za mafunzo ya ujasiriamali, Shilingi 12,300,000 utengenezaji barabara, 13,717,000 madawati 1923, Shilingi 163,455,000.

Sekta ya Elimu, Sera ya Elimu bure imefanya uandikishaji darasa la kwanza kuongezeka hadi kufikia 113%, Jumla ya shilingi 3,428,819,376 zilipokelewa katika shule zetu kwajili ya gharama za utawala katka shule zote jimboni, Ukarabati wa shule  Kongwe shilingi 825,841,642 zilizopokelewa kukarabati shule ya sekondari Bwiru wavulana madarasa 19, mabweni 11, jengo la utawala, maabara 2, maktaba 1, vyoo 9 na mfumo wa maji na umeme

Upande wa Michezo jumla ya shilingi 17,950,000 zimetumika katika kuimarisha michezo kuanzia ngazi ya shule za msingi, sekondari na mashindano ya Jimbo Cup

Upande wa miradi ya maji mikubwa imetekelezwa chini ya ufadhili wa benki ya uwekezaji ya Ulaya Euro 104.5 milioni  na Euro 14.7 milioni kutoka shilika la maendeleo la ufaransa, Miradi ambayo ikikamilika itatoa suluhu ya tatizo la maji jimboni sambamba na uchimaji wa visima 10 inaendelea vyema katika maeneo ya vijijini

Upande wa kuimarisha chama jumla ya shilingi … zilitumika kununua tairi za gari la chama, kuchangia mikutano ya chama na jumuiya zake na kuchangia ujenzi wa ofisi ya chama

Katika suala zima la uwezeshaji wananchi kiuchumi Halmashauri ya manispaa ya Ilemela imetumia Shilingi 283,000,000 kwaajili ya wanawake na vijana jumla ya vikundi 129 vimenufaika wanawake vikundi 82 na vijana vikundi 47 huku akiwaasa wananchi na viongozi kuendelea kushirikiana katika kuwaletea wananchi maendeleo

'... Ndugu zangu kwanza nawashukuru kwa kukipa ridhaa chama cha mapinduzi kuweza kushika dola, na mimi muwakilishi wenu kama inavyonitaka katiba ya chama cha mapinduzi ibara ya 73 na Ilani ya uchaguzi ibara ya 180 nina wajibu wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa ilani kwa kipindi  hiki cha miaka miwili ili mpate kujua  tumewafanyia nini kwa kushirikiana na Serikali na Viongozi wenzangu kwa maana ya mheshimiwa Rais, mbunge na madiwani ...' Alisema

Akifungua mkutano huo mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ilemela Nelson Meshack amewaambia wananchi waliohudhuria mkutano huo kuwa mkutano mkuu wa utekelezaji wa Ilani ni mkutano halali na wa kikatiba wenye lengo la kuwapa wanachama na wananchi  fursa ya kujua serikali waliyoichagua na  viongozi wao wamewafanyia kitu gani katika kuwaletea maendeleo

Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi kupitia kundi la wabunge Mhe Lusinde amewataka viongozi na wanachama wa chama cha mapinduzi wilaya ya Ilemela kuwa na moyo wa kuthamini mchango wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo unaofanywa na viongozi waliowachagua na kuwa mstari wa mbele kwa kuyasema mazuri yanayofanywa na Serikali ya chama cha mapinduzi na viongozi wake huku akikemea vitendo vya usaliti, majungu na utumiaji vibaya wa mamlaka kwa kuwagawa wanachama

Akihitimisha mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Kheri James amekemea vitendo vya baadhi ya wanachama na viongozi vya kukwamisha utekelezaji wa Ilani katika kuwaletea wananchi maendeleo na kuongeza kuwa chama cha mapinduzi hakitamvumilia mtu yeyote atakae kwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa maslahi yake binafsi sambamba na kuwaasa kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais Mhe John Magufuli na Mbunge Dkt Angeline Mabula kwa jitihada zao za kuwaletea wananchi maendeleo

Mkutano mkuu huo maalum pia ulihudhuriwa na watumishi wa umma wa Jimbo la Ilemela, taasisi za umma, mashirika binafsi, na viongozi mbalimbali wa maeneo mengine wakiongozwa na katibu wa CCM mkoa Mwanza

' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga'

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
10.04.2018

Comments