Back to top

Ujumbe wa Makamu Mwenyekiti Bara Kwa Vijana wa CCM.

03 April 2018
Share

Lusekelo na vijana wenzako wana CCM leo nawapeni ujumbe wa Pasaka ni salamu kwenu nyote Fanyeni Kazi ya Chama, si Miradi au Ujenzi au Mipango ya Serikali itawapatia kura hata km mizuri sana sana sana itaongeza joto la upinzani. 

Muelewe hivyo uhusiano kati ya Miradi ya Maendeleo na kura ya mtu kwa Chama tawala ni vigumu kupima, na kwa hakika kusimamia utekelezaji wa Ilani kwa kiasi kikubwa ni kusimamia dola itekeleze ahadi za maendeleo zilizo kwenye ilani hiyo na kwa hakika miradi hiyo kadhaa huimarisha upinzani.

 Dawa ninini - ni kufanya kazi ya Chama nje na ndani ya Umma, na kazi ya Chama ndani ya Chama - msikalie na mmbweteka na slogans tuu - kidumu, zidumu, kidumu Chama cha Mapinduzi - mtapigwa bao - tena kwa fitina yenu wenyewe ubinafsi, makundi na kutaka vyeo ili kupiga - someni historia ya Vyama vikubwa vilivyoanguka.

 Chama cha kikomunisti USSR - na sera zao za maendeleo - war communism halafu New Economic Policy ikafutia Stalinism - ni kweli ilijenga maendeleo USSR na kuwa Taifa kubwa duniani lkn wakasahau kazi ya Chama - wateule wachache wakawa Chama - msukosuko uliotokea - vikasambaratika vyote Chama na Taifa - miradi ya maendeleo ina tabia ya kuelimisha wananchi na rika jipya la wananchi na wanasiasa: 

Nitakupeni mfano toka 2005 tulipopata 80% na kidogo ya kura sera yetu shule kila kata,  barabara kuunganisha mikoa lami na fikiria UDOM tukaanzisha sisi tukawa tumekalia iena iena CCM nambari one bila kufanya kazi ya Chama - UDOM ikawa mahali kambi ya wapinzani : 

Na kwa hakika kura zetu zimekatwa km hatuoni kwa 30% na kwa hakika uchaguzi ni 50/50 itategemea kazi ya Chama na pia aina ya mgombea - sababu ya msingi wana CCM mmekalia mipasuko na kufanya kazi za dola - huko ndiko kunalipa - msaidieni Mwenyekiti. kura ingawa inachangiwa na miradi lkn ili uipate ni lazima umfikie mwananchi ni imani kama sala hujengwa kuna ijumaa/Jumapili ngapi kwa mwaka waumini wanakutana kuaminishwa jambo lile lile -

 Mungu yupo - kazi ya Chama ndani na nje ni ya kudumu kuwaaminisha watu kama CCM inachagulika kwa sababu itikadi, imani na siasa yake ya Ujamaa na Kujitegemea inawajali wanyonge na kwa sababu Kidumu CCM,  kidumu Chama Tawala - tutapigwa - maendeleo mengi elimishi mijini na vijijini huwafungua vijana na wananchi kutafuta mabadiliko pamoja na ya siasa.

 Tathmini ya Mwaka 2010 ilitufungua macho majimbo zaidi ya 10 na kati ya 28 ya makao makuu ya mikoa ubunge ulienda upinzani kwa mara ya kwanza - na au tofauti ya kura kati ya mgombea wa CCM na upinzani ni ndogo - 

Lakini bado tukaendelea business as usual - makundi ya kupiga ubinafsi - Kidumu Chama Tawala - walahi tutapigwa ktk sanduku la kura na hatutarudi tena - UZOEFU WA KIHISTORIA UMEONYESHA HIVYO -

 Hii ndiyo salamu yangu ya Pasaka kwa wana CCM wenzangu - MUNGU AKUBARIKI

Comments