Back to top

MWENYEKITI UVCCM TAWI LA MZAMBARAUNI AKABIDHI KADI WANACHAMA WAPYA

11 April 2018
Share

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tawi la Mzambarauni kata ya Chamazi,Ndg.Ally Muhunzi jana Apr 08, 2018 amekabidhi kadi kwa wanachama wapya wa uvccm na shilingi milioni moja(1,000,000/=), kwa timu ya Rede ya tawi hilo. 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Ndg.Muhunzi amewataka vijana  kujitambua na kujikita kwenye siasa ya maendeleo.

"Nawapongeza sana vijana wangu,kikubwa nataka mjitambue na kujua kuwa kuna maisha baada ya siasa" alisema Muhunzi

"Nitawakabidhi shilingi milioni moja pesa hizi nataka ziwanufaishe ninyi kwa kuanzisha miradi midogo midogo ya maendeleo ili muwe wajasiliamali,pia nitahakikisha namtafuta mtaalamu wa ujasiriamali na kuandaa semina ili vijana mpate elimu ya ujasiriamali" alisema Muhunzi.

"Ninacho waomba pesa hizi zitumike vizuri kwa lengo tulikokusudia na si vinginevyo, nataka kuona kila kijana aliye kwenye tawi hili anakuwa na mafanikio bila kuchagua rangi,kabila wala dini, sisi sote ni wamoja hivyo tupendane na tushirikiane kukidumisha chama cha mapinduzi, jumuiya ya vijana na vikundi vyenu vya ujasiriamali mtakavyo vianzisha na mimi pamoja na viongozi wangu wote tunawaahidi tutakuwa pamoja"alisema Muhunzi. 

Sambamba na hilo Ndg.Muhunzi alipongeza timu ya wanawake ya Mzambarauni Queens inayo shiriki mashindano ya UVCCM CHAMAZI REDE CUP kwa kufuzu hatua  ya makundi na kuwataka wazidi kujianda kwa kufanya mazoezi ili kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano hayo.

Huku Katibu wa tawi hilo Ndg.David Simba akiwataka vijana kupendana na kushirikiana.

"Vijana pendaneni kuweni kitu kimoja pia mshirikiane na viongozi wenu wote kuanzia Kata,mpaka viongozi wa Matawi muwaheshimu na kuwasikiliza"alisema Simba

"tunataka siasa iwe ya maendeleo na manufaa kwenu kama Mwenyekiti wangu alivyoseema, pia nami nawapongeza Mzambarauni Queens kwa hatua mliyofikia, tunawaahidi tutakuwa nanyi bega kwa bega mpaka hatua ya mwisho" alisema Simba. 

Naye Katibu Hamasa na Chipukizi wa tawi hilo na mjumbe wa H. Kuu ya kata  Ndg.Abdulmajidi Ngililea ametoa shukrani kwa niaba ya vijana wote na kuwataka vijana kuwaunga mkono na kuwaombea viongozi wao kwani wanafanya kazi kubwa na wanakutana na changamoto nyingi, pia amewataka vijana kubadilika na kusoma alama za nyakati.

"Shukurani sana Mwenyekiti pamoja na Katibu kwa kazi yenu kubwa mnayo ifanya, kwani kazi yenu mnayo ifanya inanifanya hata mimi majukumu yangu ya uhamasishaji kuwa mepesi na lahisi kupitia ninyi, kwenye hilo nawapongeza sana,vijana wenzangu tuwaunge mkono na kuwaombea viongozi wetu kwani wanapambana sana kwa ajili yetu" alisema Ngililea.

"Ni muda wa vijana kusoma alama za nyakati,kuchangamkia fursa na kutoka vijiweni, kwani itasaidia sana kujiepusha na vitendo viovu na visivyofaa ndani ya jamii yetu, kwani rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anatusisitiza sana vijana kufanya kazi kwa bidii na sisi kama vijana ni lazima tufanye KAZI, HAPA KAZI TU"alisema Ngililea.

Comments