Back to top

MARUFUKU KUANDAMANA - MWENYEKITI UVCCM RUFIJI

04 April 2018
Share

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rufiji Ndg.Juma Seif Kwangaya leo Apr 04,2018 Amefanya Kikao na Vingozi wa Uvccm Tarafa ya Ikwilili yenye Kata tatu,ambazo ni Kata ya Umwe, Kata ya Mgomba na Kata ya Ikwilili Kati.

Akizungumza wakati wa kikao hiko Ndg.Kwangaya amewambia Viongozi hao kuwa ni marufuku kwa vijana wa Wila ya Rufiji kuandamana na badala yake wajikite katika kufanya kazi.

"Ni marufuku kwa kijana wa wilaya hii ya Rufiji,Kushiriki,Kushawishi Mandamano kwa njia yeyote ile iwe Mitandaoni ama ile ya kujikusanya kimakundi na N.k na tutakapo baini vijana ama kikundi chochote cha vijana wameshiriki ama kushawishi tutamfikisha sehemu husika" Alisema Ndg.Kwanganya

"badala yake nataka vijana tufanye kazi kama Mh Rais wetu mpenda Dr.John Pombe Magufuli anavyo tusistizia vijana kufanya kazi ili twende sawa na speedi ya Serikali yetu ya Awamu ya Tano" Alisema Ndg.Kwangaya

Sambamba na ilo aliwataka Viongozi hao kuwajibika ipasavyo kwenye nafasi wanazo zitumikia ili watakapo maliza muda wao wa uongo wawe wameacha alama.

Pia Ndg.Kwangaya ameendelea kwa kusifia Juhudi zinazofanywa na Serikari ya awamu ya tano inayoongozwa na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Joseph Magufuli anaetekeleza vyema Majukumu yake na kuwashangaa wapinzani wanao beza Juhudi hizo.

Kikao hiko kilichohudhuliwa na Diwani viti maalum kutoka Tarafa ya Ikwilili Ndg.Lailati maalum pamoja na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Rufiji Ndg.Athumani Chadari

Imetolewa Na
Kitengo Cha Habari na Mawasiliano
Uvccm Rufiji

Comments