Back to top

Maadhimisho ya Kongamano la Kumuenzi Mwl.Nyerere

11 April 2018
Share

Katika kuadhimisha kongamano la kumuenzi Mwl.Nyerere na falsafa zake, kwa mara nyingine tena Chuo kikuu Cha Daresalam kupitia Kigoda cha Mwl Nyerere kinakuletea kongamano la siku 3 litakalofanyika Nkrumah Hall ndani ya viunga vya chuo kikuu Cha Dar es Salaam kuanzia tar 11 hadi 13, April 2018.

Mada kuu kwa mwaka huu ni "Wimbi La Uporaji Rasilimali Afrika:Wanyonge Wanajikwamuaje".

Majukwaa mbalimbali yameandaliwa kuweza kutoa fursa kwa makundi mbalimbali ya watu kuweza kujadili kwa mapana yake namna mbalimbali tunavyoweza kutetea na kunufaika Rasilimali za nchi yetu Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla wake na kujikomboa kutoka kwenye ombwe la ubepari na utumwa wa nchi za kibepari.

Ni kongamano la aina yake, burudani, maswali na majibu. Watu woote wanakaribishwa kuhudhuria na kushiriki mijadala.

Imetolewa na,
Idara ya mawasiliano
Kigoda Cha Mwl Nyerere-Udsm

Comments