Back to top

JUMUIYA YA UMOJA WA WAZAZI TANZANIA MKOA WA DAR ES SALAAM, YAADHIMISHA KWA KISHINDO MIAKA

05 April 2018
Share

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo  akimkabidhi Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) Cheti cha Skurani kutoka Umoja huo Wilaya ya Kigamboni kutambua mchango mkubwa wa hali na mali ambao amekuwa akiutoa kwa jumuiya hiyo, wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya miaka 63 ya Umoja wa Wazazi Tanzania, lililoandaliwa na Umoja huo mkoa wa Dar es Salaam, katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, leo.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akishuka katika gari lake baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, kuadhimisha miaka 63 ya kuzaliwa Umoja wa Wazazi Tanzania.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akikaribishwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba baada ya kuwasili eneo la Ukumbi wa wa Mikutan wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Lugano Mwafongo

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akisalimiana na Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, Lugano Mwafongo baada ya kuwasili eneo la Ukumbi wa wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akisindikizwa na viongozi kwenda ukumbini baada ya kuwasili eneo la Ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe, na kutoka kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa huo Lugano Mwafongo na Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Kate Kamba 

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akipata maelezo ya awali kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam Frank Kamugisha baada ya kuwasili katika chumba cha Wageni maarufu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, Lugano Mwafongo (kushoto) akiwa na Katibu wa CCM mkoa huo Saad Kusilawe wakati wa mazungumzo hayo.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiwaunga mkono wajumbe waliokuwa wakimshangilia baada ya kuwasili ukumbini kwenye Kongamano la miaka 63 ya kuzaliwa kwa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, yaliyoandaiwa na Umoja huo mkoa wa Dar es Salaam. Kulia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa dar es Salaam Frank Kamugisha.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiwa na viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, tayari kushiriki kongamano hilo

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Mwinyimkuu Sangaraza akifungua pazia la kongamano hilo kwa kufanya utambulisho

 "Jamani sare maalum ya sherehe hizi ilichelewa kidooogo, lakini ninayo imeshafika hii hapa" akasema Sangaraza na kuwaacha wajumbe na mgeni rasmi wakicheka

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala akisalimia baada ya kutambulishwa

 

 

Comments