Back to top

KINANA AWAKILISHA CCM KUSAINI NA KUTOA POLE KUFUATIA KIFO CHA WINNE MANDELA 9/04/2018

09 April 2018
Share

Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana leo ameongoza ujumbe wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na  jumuiya zake, kuzuru ubalozi wa Afrika ya kusini nchini Tanzania  kusaini na kutoa pole kufuatia kifo cha Mke wa Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini na mwanaharakati  Mama Winnie Mandela aliyefariki 2/04/2018 Johanasburg  nchini Africa ya Kusini.
                      
Katibu Mkuu amefuatana na Mwenyekiti wa UWT  Mama Caudensia Kabaka, Katibu Mkuu wa jumuiya ya Wazazi Maalim Seif Shaaba,  Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa NEC Siasa na uhusiano wa Kimataifa Kanal mstaafu Ngemela Lubinga, Naibu Katibu Mkuu wa UWT na Naibu Katibu Mkuu wa jumuiya ya Wazazi.

Comments